Ombi La Wokovu.

 

Jinsi ya Kuirithi Zawadi BURE ya Uzima wa Milele.

 

Je, Ubatizo ni Jambo Muhimu Kwa Kupata Wokovu?

 

 

*******

 

YAHUSHUA Mpendwa,

 

Nakukubali sasa kama BWANA na MWOKOZI wangu, Wewe ndiye Mungu ninayependa. Naamini ya kwamba ulilipa gharama ya dhambi zangu pale Kalvari, ulikufa na kufufuka katika siku ya tatu. Nauliza uje moyoni mwangu, nisamehe dhambi zangu, nioshe niwe msafi wa udhalimu wote. Pole kwa kutenda dhambi, na nageuka kutoka kwa dhambi hizo. Asante kwa kunijaza na Roho Mtakatifu wako, na kunipa hamu ya kukutumikia siku zote za maisha yangu, na uishi maisha yako ndani yangu YAHUSHUA, ili Utukuzwe! Asante kwa kunipa hamu ya kusoma Bibilia, na kunipa hekima niielewe. Asante kwa Kunipenda na Kuokoa roho yangu, ikisababisha Imani yangu kukua, ili siku moja nitakuwa na WEWE Mbinguni. Nijaze na Roho Mtakatifu wako sasa na niokoe kutoka kwa yule muovu katika jina lako YAHUSHUA Naomba! Nisaidie YAHUSHUA kukumbuka wote wametenda dhambi na kupungukiwa na Utukufu wa YAHUVEH, na ulikuja kutuokoa sisi watenda dhambi, ndio sababu wewe huitwa MWOKOZI wetu. Amina.

 

*******

 

Soma ombi hili alafu isome tena, wakati huu BILA maarifa ya kichwa lakini na moyo wako wote, iamini kwa IMANI, na kumbuka YAHUSHUA SI Mungu Pekee, lakini YEYE ni rafiki wako wa dhati! Anakujali sana, Anakupenda sana. Jinsi vile ulivyo. Anachukia Dhambi, lakini Anakupenda WEWE, mtenda dhambi!

 

 

YAHUSHUA alilipa gharama ya dhambi zako, sasa hufai kujisikia kama mwenye hatia au aliyehukumiwa tena! Ungama dhambi zako kwa YAHUSHUA. Zitaje, alafu mwambie pole, muulize akusamehe! Dhambi zako zote za zamani na sasa. Dhambi ni kitu chochote ulichofanya au unachofanya kinchomchukiza YAHUVEH Mtakatifu. Hakuna mtu aliye bora zaidi kushinda mwingine! Kumbuka haya!

 

Soma Agano Jipya ili upate kujua YAHUSHUA ni nani. (Yohana 3:16) Bibilia husema lazima umwungame Yeye kama BWANA na Mwokozi ili Akuungame mbele yake Baba. Usione aibu kumjua YAHUSHUA, kwani Yeye HAONI aibu kukujua WEWE. Ambia mtu ya kwamba umemkubali YAHUSHUA wa Kalvari na Nazareti, siku hii na malaika wote mbinguni wanashangilia.

 

 

Turuhusu tushangilie nawe. Kama unahitaji Mchungaji, tuna wengi zaidi ya mmoja. Karibu katika Familia ya YAHUSHUA! TUNA MATUMAINI YA KWAMBA TUTAKUTANA NAWE MBINGUNI, KAMA SI HAPA DUNIANI!

 

Tuma Barua Pepe kwa Elisabeth na umueleze juu ya zawadi ya uzima wa milele ambayo umerithi kutoka kwa YAHUSHUA Masihi wetu Mpendwa!

 

revholyfire@hotmail.com

 

*******

 

Rudi Kwa Ukurasa Wa Wokovu

Je, Ubatizo ni Jambo Muhimu Kwa Kupata Wokovu?

Ubatizo, Mto wa Yordani

 

Mbatizwe. (Ona Matendo ya Mitume 2:38, 39)

 

Kubatizwa inamaanisha kutumbukizwa kwenye maji. Wakati mwingine, mtu husimama ndani ya maji alafu hutumbukizwa majini (na Mkristo mwenzake) kisha huinuliwa kutoka majini na kusimama tena. Umuhimu wa kitendo hiki unaonekana katika Kitabu cha Warumi 6:1-7 na zoezi hili hupatikana katika Kitabu cha Matendo ya Mitume 8:26-39.

 

Watu wengine hufikiria ya kwamba ubatizo si moja ya vitendo ambavyo ni ishara ya kumkubali YAHUSHUA. Hata hivyo, jambo moja ni wazi katika Bibilia. Imani na ubatizo huwa pamoja kila wakati, hazijatenganishwa. Kwa hivyo, ni wazi ya kwamba Ubatizo ni ishara ya kumkubali YAHUSHUA. Tunawahimiza wote mtafute sababu za ubatizo katika Bibilia. Mkristo yeyote wa kweli anaweza kukubatiza.

 

Kubatizwa na maji ni njia moja. YAHUSHUA alisema, “Yohana alibatiza na maji lakini YAHUSHUA hubatiza na MOTO wa ROHO MTAKATIFU!” Baada ya kubatizwa na maji, ULIZIA kujazwa kwa MOTO wa ROHO MTAKATIFU! Hivi ndivyo zawadi za ROHO MTAKATIFU hupatikana! Kwa hivyo, usiamini ya kwamba KAMA hauna hizi zawadi au huwezi kuzungumza katika ndimi takatifu, hautaenda Mbinguni! Hili ni funzo la uongo! Jambo hili lingekuwa kweli, basi YAHUVEH angesema vivyo hivyo kwa uwazi ya kwamba wote ambao hawawezi kuzungumza katika ndimi takatifu HAWATAOKOLEWA! Tena, lingekuwa kweli, hakungekuwa na haja ya YAHUSHUA kupeana maisha yake na kumwaga damu pale Kalvari! Ni Damu yake YAHUSHUA Pekee inayoosha dhambi zote kwa wale wanaokubali ZAWADI hii kwa IMANI!

 

Kanisa zingine hufunza KAMA mtu hajabatizwa, hata mtoto mdogo, basi huyo mtu hataenda Mbinguni! Jambo hili lingekuwa kweli, kwa nini basi YAHUSHUA alijitolea pale Kalvari? Ubatizo ni ishara wazi kwa wote kuona ya kwamba tunamfuata YAHUSHUA! Watoto wadogo hawawezi kuyaelewa haya vizuri, kwa hivyo HAIFAI kuwabatiza mpaka watakapoweza kuelewa gharama ambayo mtu anafaa kulipa ili kumfuata YAHUSHUA. Inafaa watoto wachanga waletwe mbele yake Baba wanapozaliwa, SI kuwabatiza, kwa sababu lazima waamue wenyewe wakiwa wamekua.

 

Kwa hivyo, badala ya kuangalia ubatizo kama kitu ambacho LAZIMA ufanye, bali na kumkubali YAHUSHUA kama Bwana na Mwokozi wao, ili waokolewe… lazima mtu ATAKE kufanya jambo hili, ili kuruhusu kujazwa kwa Roho Mtakatifu na kuonyesha kila mtu ya kwamba wana uhusiano na kifo na kufufuka kwa Mwokozi wao, YAHUSHUA Ha Mashiach!